Kuhusu sisi

Tunaboresha Biashara

 

 Nauza ni mpango maalum wa kuboresha biashara ndogo na za kati kwa kuwaunganisha na mfumo mahsusi wa kusimamia biashara. Tunalenga hasa sehemu za mauzo, ambapo tunazipatia biashara na mfumo wa mauzo (Point of Sale) ambao umechangamana na mifumo mbalimbali maalum ya kusimamia biashara.

Kwa kutumia Nauza, biashara zinaweza kusimamia taarifa zote kwa usahihi na umahiri zaidi kuanzia idadi na aina ya bidhaa walizonazo, wasambazaji, wateja, mauzo, masuala ya fedha na mambo mengine yote yanahosu biashara.

We are committed to providing the right combination of management tools for businesses. By using the Nauza platform, you will be able to better manage all the critical areas of your business and discover new ways to increase your revenue. We want to help you keep better track of your business. We want you to focus more on operations and never worry about software.
Tumejipanga kuzipatia biashara na mifumo sahihi ya usimamizi. Kwa kutumia Nauza, utaweza kusimamia maeneo yote muhimu ya biashara yako kwa umahiri zaidi. Tunapenda utumie muda wako kwenye kufanya biashara yako kwa ufanisi na usiwe na hofu tena na mifumo ya usimamizi.

Sisi ni kina nani?

Nauza ni mradi unaosimamiwa na kumilikiwa na THEDEXTAZLAB Studios, wabunifu na waundaji mahiri wa mifumo kutoka Arusha, Tanzania.